come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

CAF YAGOMA KUSIMAMISHA MICHUANO SABABU YA EBOLA



Shirikisho tawala la kandanda barani Afrika, Caf limetofautiana na wenyeji Morocco huku wakishikamana kuwa dimba la mataifa bingwa la 2015 litaendelea kama ilivyopanga licha ya nchi andalizi kuelezea hofu ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Morocco waliomba shindano hilo liahirishwa kufuatia mkurupuko wa ugonjwa huo ambao umeua watu zaidi ya 4,000 baada ya maafisa wa afya nchini humo kuonya kuendelea kwa dimba hilo linalo husisha mataifa 16 kunaweza kuendeleza uambukizaji zaidi.

Mshauri wa Waziri wa Michezo wa Morocco, Mohammed Ouzzine, alieleza taifa hilo la magharibi mwa bara hilo lina wasiwasi kuandaa shindano hilo linalochukua wiki tatu.

“Matakwa ya Morocco na wakaazi wake pamoja na wale wa bara Afrika yanadunisha linguine lolote. Morocco wamewasilisha ombi hilo kufuatia ushauri muhimu kutoka maafisa wa afya.


“Hatuwezi hatarisha maisha ya watu kwa kuendelea kuandaa shindano hili kwani msingi wa tahadhari unafaa kufuatwa,” mshauri Hamid Faridi aliambia stesheni ya redio, Atlantic Jumamosi.
Kwa majibu, Caf walitoa taarifa wakitofautiana na wenyeji hao huku Afrika Kusini wakilengwa kama waandalizi wa dharura ikiwa Morocco watajiondoa.

“Caf wanadhibitisha hakuna badiliko kwenye ratiba ya shindano hili. Tungependa kukumbusha kwamba tangu dimba la kwanza la 1975, shindano hili halijawahi chelewa au kuhairishwa,” taarifa ya utawala huo wa kandanda ilisema.

Mataifa ya Afrika magharibi, Guinea, Liberia na Sierra Leone yameadhirika zaidi na mkurupuko wa sasa wa Ebola. Guinea na Sierra Leone bado wanawania tiketi za Morocco 2015.
Afrika Kusini waliokoa jahazi la shindano hilo 1996 na mwaka jana.