![]() |
|
|
|
Shirikisho la kandanda barani Ulaya, Uefa
limempiga marufuku rais wa mchezo huo nchini Italia, Carlo Tevecchio,
kutoka kongamano lao lijalo na kumwagiza aandae hafla ya kupinga ubaguzi
wa rangi kama adhabu ya matamshi aliyotoa.
Katika taarifa, utawala huo wa Ulaya ulitangaza kuwa kitengo chao cha maadili kiliamua kutoa adhabu hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi ulioanza mwezi Agosti.
Tavecchio, 71, amekatazwa kuhusika katika shughuli zozote rasmi za Uefa akisubiri uamuzi zaidi kuhusu sakata iliyo tokea baada ya kusema kwenye kampeni za uchaguzi wa kiongozi wa soka nchini humo kuwa vilabu vya Italia vinasajili “Opti Poba (weusi) waliokuwa wanakula mandizi hapo zamani lakini kwa ghafla wanajipata kama wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Lazio.”
Mtamshi hayo yalioonekana kulengwa kwake kiungo wa Ufaransa anayechezea mabingwa wa Serie A Juventus, Paul Pogba, ambaye ni mweusi huku wengi nchini Italia wakiyakemea kama shambulizi la ubaguzi wa rangi.
Uefa walisema Tavecchio, 71, “amekatazwa kushikilia wadhifa wowote kama afisa wa shirikisho hilo kwa miezi sita kutoka tangazo hili na wala hatahusika na kongamano la Uefa la Machi 24, 2015.”
“Bwana Tavecchio ata andaa hafla spesheli Italia inayonuia kuhamasisha na kufuata kanuni zilizoko kutokana na kampeni ya UEFA ya Kandanda dhidi ya Ubaguzi wa Rangi,” utawala huo ulifafanua.
Shirikisho la Italia, FIGC lilisema Tavecchio amekubali adhabu hiyo ili kuzuia mtafaruku zaidi na UEFA.