|
|
Mshambuliaji wa pembeni wa Uingereza, Theo
Walcott, ameingia mazungumzo ya kandarasi mpya na Arsenal baada ya
kurejea kutoka jeraha wikendi iliyopita.
Hivi karibuni, nyota huyo ataingia miezi 18 ya mwisho wa mkataba wa sasa hali ambayo imefanya miamba hao wa London kuzindua majadiliano ya kuongezea muda wa mkataba unaoripotiwa kumlipa pauni 100,000 kwa wiki.
Walcott alitumika kama mchezaji wa akiba kwenye ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Burnley Jumamosi baadas ya kureja kutoka jeraha mbaya lililompata mwanzoni mwa mwaka huu.
“Tutaketi naye kwasababu atakuwa katika hali yake ya juu miaka ijayo na sasa anasalia na mwaka mmoja na nusu kwenye kandarasi ya sasa. Si kazi rahisi kujadiliana na maswala kama haya ndiyo maana tumeanza mapema,” meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alidhibitisha.
“Kwa sasa, ako na umri wa miaka 25 na tunatumahi kufaidika na huduma zake kwa muda mrefu zaidi,” aliongeza.