Simba rasmi imemfungashia virago kocha wake Patrick Phiri na nafasi yake inachukuliwa na Goran Kopunovic raia wa Serbia.
Kopunovic anaingia kwenye rekodi ya Waserbia waliowahi kuifundisha Simba akiwemo Milovan Cirkovic.
Taarifa za ndani ya Simba zinaeleza Mserbia anatarajia kuwasili nchini Jumatano na Phiri ameishapewa taarifa hiyo.
Kuponovic aliwahi kuinoa Polisi Rwanda kwa mafanikio makubwa na kuiwezesha kuwa tishio mbele ya vigogo APR na Rayon.
Nafasi ya Kocha ya Msaidizi, kuna taarifa Simba ilifanya mazungumza na na Jean Marie raia wa Rwanda aliyewahi kuipa Atraco na Rayon ubingwa wa Rwanda kwa nyakati tofauti.
Lakini hata hivyo inaonekana wameshindwa kuelewana na Selemani Matola anaendelea kuitumikia.