Meneja wa Newcastle United Alan Pardew amepewa ruhusa ya kuzungumza na na viongozi wa Crystal Palace katika mpango wa kujiunga nao.
Crystal Palace walimtimua Meneja wao Neil Warnock na sasa wanataka kumchukua Pardew ili kuwa bosi mpya wa timu hiyo.
Pardew hatokuepo kwenye mazoezi ya timu yake kocha msaidizi John Carver, ndio ataongoza mazoezi ya timu ya Newcastle.
Maamuzi wa mwisho kuhusu Pardew utajulikana baada ya mazungumzo yatakayofanyika kati ya mmiliki wa Newcastle Mike Ashley na Mwenyekiti Mwenza wa Crystal Palace Steve Parish.
Kabla ya kuwa kocha wa Newcastle, Pardew aliwahi kuwa kuzifundisha timuza Reading, West Ham, Southampton na Charlton.
Alan Pardew aliwahi kuwa mchezaji wa Crystal Palace katika msimu wa Mwaka 1987 mpaka 1991.