|
|
Nahodha na straika wa Manchester United, Wayne
Rooney, ameshauri ligi ya Premier ya Uingereza ifikirie upya ratiba ya
musimu wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya ambayo huwa na shughuli
mingi.
Rooney, anasema hatari ya wachezaji kupata majeraha mabaya kwa kukosa muda tosha kupumzisha misuli ni sababu tosha ya kuchunguza ratiba ya kipindi hicho huku daraja kuu la kandanda ya Uingereza ikisalia pekee barani Ulaya kuendelea kipindi chote cha kuadhimisha Krismasi.
Wikendi iliyopita, vilabu vyote 20 vilivyohusika vilicheza mechi mbili kwa muda wa siku sawia huku wote wakijitosa uwanjani Januari 1.
Rooney aliyeanza mechi zote Ijumaa na Jumapili anaonelea maslahi ya usawa ya wachezaji yanafaa kutiliwa maanani wakati wa kupanga ratiba za mechi.
“Si rahisi kucheza mechi mbili ndani ya siku mbili kwani ubora hupotea kutoka timu mbili husika. Ni vigumu kwani tulianza vyema kipindi cha kwanza lakini cha pili kilikuwa na matatizo tele na ni matumaini yangu mambo yatabadilika siku zijazo.
“Pengine itachukua mchezaji kupata jeraha mbaya sana kwa kucheza mechi mbili ndani ya siku mbili kubadilisha mawazo ingawa hatuombei hilo lifanyike,” nyota huyo alinena.