come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PLUIJM- YANGA ITABEBA KOMBE LA MAPINDUZI

KOCHA mkuu wa Yanga SC Mholanzi Hans Van der Pluijm amesema kikosi chake lazima kiibuke na ubingwa wa michuano hiyo ili iwe zawadi kwa mashabiki wake waliokuwa hawana furaha tangia aondoke katika kikosi hicho.

Pluijm ameyasema hayo leo wakati timu yake jana kabla hawajaingia uwanjani kuikabili Shaba katika mchezo wa kukamilisha ratiba kundi A.

Alisema haoni sababu ya kikosi chake kushindwa kutwaa ubingwa huo, Pluijm amesema ameziona timu zote zinazoshiriki michuano hiyo na kudai ni timu moja tu ndio ambayo inaweza kuleta ushindani kwake lakini wataifunga tu kwa kutumia uzoefu wa washambuliaji wake.


Ameitaja timu hiyo ni KCCA ya Uganda ambayo ni timu inayocheza soka la kueleweka lakini washambuliaji wake hawako makini hivyo watatumia nafasi hiyo kuiangamiza, Yanga kwa sasa ndio timu yenye fowadi kali kwani ikiwa imecheza mechi mbili tu tayari imefunga magoli 8.