BEKI na nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kuwa ukuta wa timu yake haupitiki na tayari wameshaufanyia marekebisho madogo hivyo washabiki wa Yanga wategemee furaha tu.
Akizungumza kwa njia ya simu na Afrika Soka, nahodha huyo anayecheza kiundava amesema ukuta wao umeimarika na hakuna mshambuliaji atakayekatiza kwenye lango lao.
'Sisi mabeki tukicheza legelege tunaweza kuruhusu magoli na mashabiki wakaanza kumlaumu kipa wetu wakati matatizo tunayo sisi wenyewe, kwahiyo tumekaa na kuelewana ambapo kila mmoja tumempa makujumu ya kumlinda kipa wetu', alisema na kuongeza.
'Ninaamini kwa ushirikiano uliopo na mabeki wenzangu basi hatutaruhusu hata bao katika mechi zijazo za robo fainali na kuhakikisha tunapeleka kombe Jangwani.