Kocha wa Machester United Louis van Gaal amesema kuwa ushindi wa mabao matatu iliyoupata timu yake dhidi ya Tottenham ni jambo kubwa na akasema walipaswa kushinda baada ya kutupwa nje ya FA Cup na wapinzani wao wakubwa Arsenal.
Goli la Marouane Fellaini, Michael Carrick na Wayne Rooney yalitosha kabisa kuwapa Mashetani wekundu pointi tatu muhimu na kuendelea kujikita katika nne bora ya msimamo wa ligi. Chelsea bado wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 64, huku Manchester City wakishika nafasi ya pili kwa pointi 58, washika bunduki Arsenal nafasi ya tatu kwa jumla ya pointi 57 huku nafasi ya nne ikiwa mikononi mwa Manchester United na pointi zao 56 kibindoni.
Ligi hiyo itaendelea tena leo ambapo Liverpoool itakuwa ugenini kukabiliana na Swansea.