KOCHA mkuu wa Mtibwa Sugar Meck Mexime ameshutumiwa vikali na mashabiki wa soka kwa kitendo chake cha kumtoa mapema straika wa kutegemewa wa timu hiyo ya Turiani Mussa Hassan Mgosi ambaye alikuwa mwiba kwa mabeki wa Simba na kusababisha timu hiyo kufungwa bao 1-0.
Wakizungumza kwa vipindi kadhaa mashabiki hapo waliofurika uwanja wa Taifa kutazama mchezo huo wa ligi kuu bara ambao Mtibwa Sugar walikubali kufungwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa raia wa Uganda Emmanuel Okwi.
Mashabiki hao wamedai Mtibwa Sugar ilikuwa na nafasi pekee ya kuifunga Simba tangia mwanzo lakini mabeki wa imba walikuwa imara kuzuia hatari hizo, lakini kuwepo kwake kwa mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi ambaye alikwahi kuichezea Simba kulipelekea Mtibwa kulisakama lango la Simba mara kwa mara.
Hadi mpira unakwisha viongozi wa Simba walimfuata Mgosi na kumweleza kuwa ndiye mchezaji pekee waliyekuwa wakimuogopa, lakini kitendo cha mwalimu wa Mtibwa Sugar Meck Mexime kumtoa Mgosi hakikuwa cha kiungwana kwani kilisababisha timu hiyo kupoteza mchezo.
Mgosi alikuwa akiisaidia sana Mtibwa lakini tunamshangaa kocha amemtoa wakati timu yake ilikuwa inashambulia muda wote huku mabeki wa Simba walilazimika kumchunga yeye ambapo ingekuwa nafasi pekee kwa washambuliaji wengine kufunga