Na mwandishi wetu
KILIKUWA NI KITUKO TU! kiungo mkabaji wa mabingwa wa soka nchini Jonas Gerrard Mkude jana alitinga uzi unaovaliwa na mabingwa wa soka Afrika mashariki na kati Yanga katika mazishi ya mjomba yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni.
Kwa mujibu wa mwandishi wa kituko hiki ambaye alikuwepo katika mazishi hayo, Jonas alivalia jezi ya timu ya taifa ya Brazil yenye rangi zinazofanana na za Yanga ambazo ni njano na kijani.
Mkude ambaye hakuwa na wasiwasi wowote juu ya kuvaa kwake jezi hizo huku akiwa na majonzi kufuatia kifo cha mjomba yake aliyefahamika kwa jina George Ambrose Shimmba ambaye amezaliwa tumbo moja na mama yake mzazi.
Lakini ni habari ya kweli ila ya kufurahisha