Na Anko Matua
LICHA ya kulimwa barua mbili na uongozi wa klabu ya Simba, Kiungo nyota wa timu hiyo Mwinyi Kazimoto ameushangaa uongozi wa klabu ya Simba kwa kitendo chake cha kumhusisha na watovu wa nidhamu.
Kazimoto amesema kuwa naishangaa sana klabu yake kutokana na kumuandama na kumwandikia barua za kumuonya wakati yeye si mtovu wa nidhamu na kikubwa zaidi alikua akiumwa.
Pia anashangaa uongozi wake huo kutilia shaka habari zinazoandikwa kwenye magazeti kadhaa ya michezo hapa nchini kuwa yeye yuko mbioni kuihama klabu hiyo na kujiunga kwa watani wao wa jadi Yanga.
Kazimoto amekanusha habari hizo na kuwataka viongozi wa Simba kutopenda kufanya kazi na magazeti, kabumbu1935blogspot.co imezinyaka