Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba SC Alhaj Ismail Aden Rage hatimaye amekubali yaishe baada ya kukubali kuitisha kikao cha dharula.
Akizungumza na KABUMBU SPOTI Rage amesema kwamba mkutano wa wanachama wote wa Simba sasa utafanyika mapema hivi karibuni na si mwezi julai kama alivyonukuliwa na vyombo vya habari.
Amesema kuwa ameamua kuwakubalia wanachama wa Simba ili kujenga mshikamano ambao ulianza kupotea, Aiodha mwenyekiti huyo amedai kuwa amepokea kwa mikono miwili barua ya kuomba kujiuzuru kwa makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange 'Kaburu' lakini amegomea kujiuzuru kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hanspope.
Rage ameongeza kuwa Hanspope bado mtu muhimu ndani ya Simba hivyo atamshawishi aendelee kukitumikia cheo chake, Lakini amekubali kujiuzuru kwa Kaburu kutokana na kiongozi huyo kuandamwa na wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba ambao walipinga kuwepo kwake tangia mwanzo