Na Poul Mokiwa
STAA wa kike kwenye kiwanda cha filamu bongo ama Bongo Movie El;izabeth Michael Kimemeta a k a Lulu ambaye hivi karibuni aliachiwa kutoka mahabusu ya gereza la segerea anatarajia kurejea kwa kishindo kwenye tasnia hiyo imebainika.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu ambaye aliitonya KABUMBU SPOTI inasmekana Lulu atarejea kwenye filamu na huenda akavunja rekodi ya mauzo kutokana na shauku ya wapenzi wa filamu kutaka kumuona mwanadada huyo kwa mara ya kwanza tangia alipotoka lupango.
Mtu huyo ambaye ndiye chanzo chetu cha habari amesema kwamba Lulu atakuwa kivutio kikubwa atakaporejea, ameongeza kuwa wapenzi na mashabiki wa filamu wanataka kumuona Lulu baada ya kutoka sero ambapo alikamatwa baada ya kutuhumiwa kumuua kwa bahati mbaya gwiji la filamu nchini Steven Kanumba 'The Great'.
Hata hivyo bado Lulu ajathibitisha kama kwel;i atarejea kwenye filamu kufuatia taharifa za awali kusema kuwa huenda msanii huyo akaachana na filamu na kujikita kwenye elimu