Na Mwandishi Wetu
KIUNGO mshambuliaji wa mabingwa wa soka Afrika mashariki na vinara wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Haruna Niyonzima amenakusha uvumi wa kujiunga na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Simba SC mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Niyonzima amekanusha uvumi ulioenea jijini kuwa ana mpango wa kusajili Simba baada ya kuchoshwa na Yanga, Nyota huyo aliyegeuka mfungaji muhimu hivi karibuni kwa klabu yake ya Yanga amesema taharifa zinazoenezwa juu yake ni uongo.
'Sina mpango wa kujiunga na Simba najua hayo ni maneno ya watu wanaopenda kueneza taharifa za uongo ili wasikike', alisema kiungo huyo anayesifika katika ukanda huu wa Afrika mashariki.
Hivi karibuni kiungo huyo aliingia matatizoni na klabu yake ya Yanga ambapo alikuwa akishindwa kuripoti kambini kuungana na wenzake, Niyonzima alishindwa kuitumikia klabu yake katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Morogoro ambapo Yanga ilibanwa mbavu baada ya kulazimishwa kwenda suruhu ya 0-0 na kuwakatisha tamaa mashabiki wake ambao wanashauku kubwa na ubingwa wa bara