come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NYAMLANI KUMUHUKUMU LADY JAYDEE

(Pichani) Lady Jaydee
Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini , Judith Wambura 'Lady Jaydee' jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo.


Katika hati ya madai hayo, Jaydee anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamlani Mei 27 mwaka huu.   

Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao waliwakabidhi hati ya mashitaka hayo. 

Jaydee ambaye alikuwa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) akiongea katika Jukwaa la Sanaa, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake. 

Jambo pekee alilosema kwa waandishi ni kwamba, kesi itaanza kunguruma mahakamani hapo Mei 27. 

Miongoni mwa vielelezo alivyopewa na mahakama ambavyo alivionesha kwa baadhi ya waandishi ni pamoja na nakala za magazeti na nakala za 'post' za blog yake pamoja na ujumbe aliokuwa akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa za mwanadada huyo kufikishwa mahakamani hapo, ziliibuka chinichini kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo baadaye Lady Jaydee alihoji kuwa pengine yeye ndiye anayestahili kuwapeleka mahakamani wasanii walio chini ya Tanzania House of Talent (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ na Elias Barnaba ambao anadai aliwalipa kianzio cha shoo yake ya Mei 31, mwaka huu kisha 'kumchomolea' dakika za mwisho kushiriki.

Jaydee aliposti katika blog yake ya ladyjaydee.blogspot.com waraka mrefu akiitaka radio Clouds FM isipige nyimbo zake na hata ikitokea ametangulia kufa isitangaze habari yoyote ya kifo chake na kwamba viongozi wa Clouds wasihudhurie hata msibani huku akiwataka watakaokuwapo msibani wawapige mawe wawili hao endapo watahudhuria.
Chanzo: Mpekuzihuru.com