KLABU ya Barcelona imepata ushindi
mwembamba wa 1-0 dhidi ya Malaga jana na kuendeleza mwanzo wao mzuri
katika mbio za kutetea taji lao la La Liga.
Mabingwa hao walimkosa majeruhi Lionel
Messi na ilisota kupata bao hilo pekee hadi beki wa pembeni Adriano
alipokatiza upandd wa kulia kuingia ndani kabla ya kufumua shuti kali
lililotinga nyavuni kabla ya mapumziko.
Mshambuliaji Mbrazil, Neymar aliingia kipindi cha pili na kuonyesha alistahili kuigharimu Barca Pauni Milioni 50.
Nyota kinda: Mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 50, Neymar aliingia kipindi cha pili na kufanya vizuri
Hasira: Sergio Sanchez wa Malaga akionyesha hasira zake baada ya timu yake kukosa bao la wazi
Kasi: Alexis Sanchez wa Barca akimtoka Vitorino Antunes wa Malaga
Kazi kazi: Beki wa Malaga, Jesus Gamez alipewa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Neymar
Tabasamu: Gerardo Martino baada ya ushindi jana