Klabu ya soka ya Uturuki,
Fenerbahce, imepigwa marufuku ya kushiriki katika michuano ya bara Ulaya
msimu huu, baada ya mahakama ya upatanishi ya michezo CAS, kuidhinisha
uamuzi uliokuwa umetolewa na shirikisho la UEFA kuwa klabu hiyo
ilihusika na sakata ya kupanga matokeo ya mechi.
Klabu hiyo ilikuwa, tayari kujiunga na ligi hiyo ya daraja ya pili, baada ya kuondolewa na Arsenal katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Shirikisho la UEFA, liliipiga marufuku Fenerbahce mwezi Juni mwaka huu, baada ya kuwapata maafisa wa klabu hiyo na hatia ya kupanga matokeo ya mechi ili kushinda ligi kuu ya soka nchini Uturuki.