Mbali na viongozi hao waliowahi kuwa wenyeviti wa CCM, pia
watakuwapo, Salmin Amour, Amani Abedi Karume, John Malecela na Pius
Msekwa waliowahi kushika wadhifa wa Makamu wa Mwenyekiti wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Wazo la kuunda baraza la wazee lilitolewa Aprili,
2011 katika kikao cha NEC baada ya wazee kuombwa kutohudhuriwa vikao vya
CC kutokana na kuhitaji safari ndefu za mara kwa mara wakati wana umri mkubwa.
Kwa ombi hilo, NEC iliridhia mabadiliko hayo ya katiba wakati wa kikao chake kilichoketi Februari 12, 2012.
Madiwani wa Bukoba kikaangoni
Hatima ya madiwani wanane waliofutiwa uanachama
huko mkoani Kagera itafahamika wikiendi hii wakati CC itakapokutana leo.
Baada ya CC, kikao cha NEC kitafanyika kesho na keshokutwa.
Nape alisema suala la madiwani wa Bukoba litakuwa miongoni mwa ajenda za kikao cha CC.
Halmashauri ya CCM, Mkoa wa Kagera hivi karibuni
iliwafukuza uanachama madiwani hao kutokana na kushirikiana na wale wa
Chadema na CUF kupinga uongozi wa Meya wa Mji wa Bukoba, Anatory Amani.
Waliofukuzwa ni Richard Gaspar (Miembeni ), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander
Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe), Yusuf Ngaiza ambaye pia ni
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya (Kashai), Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).
Baada ya kufukuzwa, Sekretarieti ya CCM ilitoa
taarifa kupinga hatua hiyo ikisema Halmashauri ya Mkoa wa Kagera haikuwa
na madaraka ya kuwatimua madiwani hao.
Ajenda nyingine
Nape alisema ajenda nyingine za CC zitakuwa
kujadili maoni ya wanaCCM juu ya rasimu ya Katiba, hali ya kisiasa na
masuala ya utumishi. Alisema NEC itajadili ajenda moja tu ya maoni ya
rasimu ya Katiba Mpya.