come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

LEOPARD YAIZAMISHA ULINZI

Allan Wanga

Kiungo wa zamani wa kikosi cha taifa, Allan Wanga, aliweza kupepea na bao la ushindi pale mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Kenya, AFC Leopards
walipowatafuna wenzao Ulinzi Stars katika kinyang'anyiro kikali kilichoandaliwa uwanja wa Afraha Stadium, Nakuru.
Timu ya ugenini Leopards walisubiri hadi dakika mbili baada ya refa kuashiria muda wa ziada kupata goli la ushindi pale Wanga alipofaulu kuelekeza mpira wavuni baada ya kombora la mwenzake Charles Okwemba kumfikia baada ya kubusu mlingoti wa lango kwa kishindo.
Baada ya mechi hiyo, mukufunzi wa Ulinzi, Salim Ali alilalamikia refa Nassur Ndoka kwa masaibu ya kikosi chake kilicho lazimishwa kucheza mechi hiyo na wachezaji kumi pale walipowahi kadi nyekundu.
"Tazamo langu kuu kutoka mechi hii ni kwamba refa aliongoza mechi hii kwa mapendeleo ni kama kwamba katika mawazo yake, tulifaa kupoteza mechi hii. Sina tashwishi kuhusu kadi nyekundu lakini utendakazi wake ulitia shauku kubwa na ni kutokana na hilo ambapo tulishindwa kuzoa alama yeyote na alitunyima haki," Salim aliongezea.
Akibeza wachezaji wake kwa 'ushidi' walioupata Ali alizidi kushambulia Ndoka akidai kuwa alikosa kwa sababu anazozielewa yeye mwenyewe kutunuku vijana wake mikwaju ya adhabu kutokana na rafu waliochezewa na mabingwa hao wa kitambo.
"Refa aliwaonea huruma sana. Kulingana nami, alifaa kuwaondoa wachezaji wao wawili kutokana na kucheza rafu lakini hakuchukua nafasi hiyo," Salim alisema.
"Nilifurahishwa na juhudi za wachezaji wangu walivyoweza kufanikiwa kuchezea uwanja mbaya. Haikuwa mechi rahisi lakini naridhishwa na ushindi huu wa maana sana kwetu," mwenzake katika upade wa Leopards, Luc Eymael alinukuliwa akinena.
Kutokana na ushindi huo, Leopards walimiliki nafasi ya pili kwa muda na alama 30 huku Ulinzi wakibakia katika nafasi ya nne na pointi 27.