Mechi tano za mchujo za kutafuta
nafasi ya kujitosa katika hatua za makundi ya Kombe la Klabu Bingwa
barani Ulaya zilichezwa siku ya Jumatano Usiku.
Mabingwa wa Ligi ya Scotland, Celtic, walikutana na Shakhter Karagandy ambao ni bingwa wa ligi kuu ya Kazaskhatan.
Celtic ilifuzu kwa ushindi mkubwa wa mabao 3-0 dhidi ya Shakhter.
Mchezaji James Forrest alifunga bao la tatu katika dakika ya mwisho na kuwezesha Celtic kujinasua kutokana na matokeo duni ya awali katika mechi ya awamu ya kwanza ambako waliadhibiwa mabao 2-0
Huku mashabiki wakishangilia katika uwanja Celtic Park, meneja wao Neil Lenon hakuficha furaha yake, ambapo alitaja ushindi huo kama ufanisi mkubwa zaidi wa soka ambayo hajawahi hitumu katika kazi yake.
Celtic sasa imefuzu kwa raundi ijayo kwa jumla ya mabao 3-2.
Katika mechi nyengine, Real Sociedad ya Uhispania nayo imeichapa Olympic Lyon ya Ufaransa mabao 2-0.
Timu hiyo imefuzu kwa hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika miaka kumi. Mchezaji wao Carlos Vela alijitahidi kufunga mabao hayo mawili ya kihistoria .