come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

USEIN BOLT AENDELEA KUNG'ARA ZURICH

Meseret Defar wa Ethiopia amedhihirisha umaarufu wake katika mbio za kina dada za mita elfu tano pale alipomshinda Muethiopia mwenzake Tirunesh Dibaba wakati wa mashindano ya IAAF Diamond league zilizofanyika mjini Zurich.

Meseret Defar alizitimuka mbio hizo kwa muda wa dakika 14:32.83, akifuatwa na Dibaba na Mkenya Mercy Cherono, ambaye ni mshindi wa medali ya fedha katika mashindano ya dunia.
Katika mbio za mita elfu moja mia tano kwa wanaume, bingwa wa dunia Asbel Kiprop, alimaliza katika nafasi ya sita, huku mkenya mwezake Silas Kiplagat akiibuka na ushindi.
Ayanleh Souleiman wa Djiobouti akiridhika na nafasi ya pili akifuatwa na Nixon Chepseba.
Bingwa wa dunia wa mbio za mita mia nane kwa kina dada, Euinice Sum kwa mara nyingine tena aliwapiku wapinzani wake katika mbio na kudhihirisha umaarufu wake katika mbio hizo.
Sum alitumia muda wa dakika moja sekunde 58 nukta 82 naye bingwa wa zamani wa dunia Mariya Savinova wa Urussi akimaliza katika nafasi ya pili akifuatwa na Malika Akkoui.

Mabingwa waadhibiwa

Ezekiel Kemboi akiwa mashindanoni
Bingwa mwingine wa dunia aliyeangushwa katika mbio hizo za Zurich, ni Ezekiel Kemboi ambaye alimaliza katika nafasi ya kumi katika mbio za mita elfu tatu kuruka maji na viunzi kwa upande wa wanaume.
Mshindi wa medali ya fedha na shaba katika mbio za dunia Conseslus Kipruto na Mahiedine Mekhissi wa Ufaransa nao walimaliza katika nafasi ya tatu na nne mtawalia.
Hillary Kipsany Yego wa Kenya aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa dakika nane sekunde nane nukta sufuri tatu.
Katika mbio za mita mia moja bingwa wa dunia na mshikilizi wa rekodi ya dunia Usain Bolt wa Jamaica alinyakuwa nafasi ya kwanza akifuatwa na Nikcel Ashmeade vile wa Jamaica na Justin Gatlin wa Marekani.
Katika mashindano hayo ya Zurich, wanariadha kumi na watano walituzwa zawadi zao ya Almasi na dola elfu arubaini pesa taslim baada ya kushinda katika vitengo vyao.
Fainali ya pili na ya mwisho ya mashindano hayo ya IAAF Diamond League, itaandaliwa tarehe sita mwezi ujao mjini Brussels Ubelgiji.