Mabingwa watetezi, Yanga FC na Ashanti zitamenyana
uwanjani hapo katika mojawapo ya mechi za ufunguzi wa ligi hiyo
inayoanza Jumamosi kwenye viwanja saba tofauti ikiwamo ule wa taifa.
Habari za kuaminika ambazo gazeti hili lilizipata
zilieleza kuwa kuwa hadi jana mchana zoezi la ufungaji mitambo ndani ya
uwanja huo lilikuwa limeshindikana.
Chanzo chetu kilieleza kuwa, mafundi mitambo wa
Benki ya CRDB ambao wamepewa tenda hiyo walizuiliwa kufunga mitambo yao
na Wachina wanaosimamia uwanja huo.
“Mafundi hao, Bodi ya Ligi na TFF walikwenda pale
kwa lengo la kufunga mitambo hiyo, lakini walikumbana na ugumu kutoka
kwa Wachina ambao hadi leo wapo pale uwanjani,” kilieleza chanzo hicho.
Chanzo hicho kilifafanua kuwa kutokana na kukwama
huko, bodi ilichukua jukumu la kuiandikia barua Serikali ili kutoa
uamuzi ambapo inasubiri jibu.
“Tayari viwanja vyote isipokuwa ule wa Taifa na
Ali Hassan Mwinyi wa Tabora, vimefungwa mitambo hiyo tayari kuanza
kutumia tiketi za elektroniki msimu huu wa ligi,” kilieleza chanzo
hicho.
Akifafanua madai hayo, mmoja wa viongozi wa juu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye hakutaka
kuandikwa gazetini kwa madi kuwa yeye sio msemaji alisema mitambo ya
uwanja huo bado haijakamilika.
“Ni kweli watu hao walikwenda wakakutana na ugumu
huo, wakakutana na ugumu huo, seva haijakamilika hata kwa matumizi ya
uwanja hata hivyo uwanja huo ni wa kielectroniki tangu unabuniwa na
waziri atalitolea ufafanuzi hivi karibuni,” alisema.