come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA KUKUTANA JIONI HII KURUDISHA UTULIVU

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Yanga SC, inatarajiwa kuwa na kikao leo jioni kujadili kitendo cha Wazee wa klabu hiyo kumkataa Katibu mpya, Patrick Naggi kutoka Kenya.

Habari kutoka ndani ya Yanga SC, zinasema kwamba kikao hicho kitafanyika makao makuu ya klabu saa 11:00 jioni ya leo na baada ya hapo klabu itatoa tamko rasmi juu ya suala hilo.

Jana, Wazee katika Mkutano wao na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, walipinga mambo mawili yaliyofanywa na uongozi wa Manji; kuleta Mhasibu mwenye asili ya Kiasia na kuajiri Katibu mpya kutoka Kenya.

Katibu Mkuu mpya wa Yanga SC, Patrick Naggi yupo tayari nchini kuanza kazi akirithi mikoba ya Lawrence Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake.

Akizungumza na Waandishi wa habari klabuni jana, Katibu wa Baraza la Wazee la klabu, Ibrahim Akilimali alisema kiongozi yeyote ambaye anapaswa kuiongoza Yanga, lazima awe mwanachama wa klabu hiyo, hivyo uongozi umekiuka Katiba.

“Mpaka sasa sisi hatumtambui, kwani hatuna vielelezo vyake vya kuwa mwanachama wa klabu hii, endapo atatuletea vielelezo hivyo sisi tutamtambua na kumpa ushirikiano.

“Kazi za Wanayanga zitafanywa na wanachama wetu pekee na si wa nje ya klabu yetu, hatutakubali hata chembe kuona katiba yetu ikikanyagwa na viongozi wetu, tutasimama kidete mpaka mwisho kuona jambo hili halifanikiwi,” alisema Akilimali.

Alisema wao wakiwa kama wanachama wa Yanga hawatambui ajira ya raia huyo wa Kenya na anatakiwa kuondoka ndani ya saa 24 klabuni hapo.

Akilimali alisema hawataki kumuona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo.

Alimfananisha Mkenya huyo ni mtu aliyeingia kwa njia za panya katika klabu hiyo, kwa kuwa hawana mwanachama wa aina yake kwenye leja ya wanachama wa Yanga.

Alisema wamekuwa na kawaida ya kupewa taarifa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Alhaj Yussuf Manji kama kunakuwa na jambo lolote ambalo wamepanga kulifanya kwa maslahi ya Yanga, lakini hawakuambiwa kuhusu ajira ya Mkenya huyo.KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Yanga SC, inatarajiwa kuwa na kikao leo jioni kujadili kitendo cha Wazee wa klabu hiyo kumkataa Katibu mpya, Patrick Naggi kutoka Kenya.

Habari kutoka ndani ya Yanga SC, zinasema kwamba kikao hicho kitafanyika makao makuu ya klabu saa 11:00 jioni ya leo na baada ya hapo klabu itatoa tamko rasmi juu ya suala hilo.

Jana, Wazee katika Mkutano wao na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, walipinga mambo mawili yaliyofanywa na uongozi wa Manji; kuleta Mhasibu mwenye asili ya Kiasia na kuajiri Katibu mpya kutoka Kenya.

Katibu Mkuu mpya wa Yanga SC, Patrick Naggi yupo tayari nchini kuanza kazi akirithi mikoba ya Lawrence Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake.

Akizungumza na Waandishi wa habari klabuni jana, Katibu wa Baraza la Wazee la klabu, Ibrahim Akilimali alisema kiongozi yeyote ambaye anapaswa kuiongoza Yanga, lazima awe mwanachama wa klabu hiyo, hivyo uongozi umekiuka Katiba.

“Mpaka sasa sisi hatumtambui, kwani hatuna vielelezo vyake vya kuwa mwanachama wa klabu hii, endapo atatuletea vielelezo hivyo sisi tutamtambua na kumpa ushirikiano.

“Kazi za Wanayanga zitafanywa na wanachama wetu pekee na si wa nje ya klabu yetu, hatutakubali hata chembe kuona katiba yetu ikikanyagwa na viongozi wetu, tutasimama kidete mpaka mwisho kuona jambo hili halifanikiwi,” alisema Akilimali.

Alisema wao wakiwa kama wanachama wa Yanga hawatambui ajira ya raia huyo wa Kenya na anatakiwa kuondoka ndani ya saa 24 klabuni hapo.

Akilimali alisema hawataki kumuona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo.

Alimfananisha Mkenya huyo ni mtu aliyeingia kwa njia za panya katika klabu hiyo, kwa kuwa hawana mwanachama wa aina yake kwenye leja ya wanachama wa Yanga.

Alisema wamekuwa na kawaida ya kupewa taarifa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Alhaj Yussuf Manji kama kunakuwa na jambo lolote ambalo wamepanga kulifanya kwa maslahi ya Yanga, lakini hawakuambiwa kuhusu ajira ya Mkenya huyo.