come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

P-SQUARE WAFANYA BALAA BONGO.

Wasanii  wakali wa kukamua jukwaani, Kundi la P Square, juzi usiku walionyesha wanastahili kukubalika Afrika na duniani kote baada ya kuliteka jukwaa katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kuweka rekodi ya kukamua kwa muda mrefu bila kuchoka.

Wasanii hao mapacha, Peter na Paul Okoye walikamua jumla ya nyimbo 11 jukwaani zikiwamo Bizzy Body, No Easy na Ifunanya, na baadaye kuwakosha Wabongo kwa kuwapa ladha ya kiswahili baada ya kushusha kibao cha wasanii wa Uganda, Radio & Weasel unaokwenda kwa jina la Nakudata.

Mashabiki waliohudhuria tamasha hilo walikiri kukunwa na shughuli hiyo pevu iliyofanikishwa na EATV kwa udhamini wa Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom baada ya kundi hilo kutumia takriban dakika 138 jukwaani 'wakikamua'.

Baada tu ya kutua nchini, P Square ambao mara baada ya 'shoo' hiyo walikwea pipa na kurudi kwao, kati ya mambo ambayo waliahidi  ilikuwa ni kuwachosha mashabiki watakaohudhuria kwa kukamua kwa saa mbili bila ya kupumzika.

Walisema: “Tutatumia saa mbili jukwaani, ambao mtahudhuria mtachoka wenyewe,” alisema Peter, jambo ambalo walidhihirisha walipopanda stejini juzi, Jumamosi usiku.


Shoo hiyo ilianza majira ya saa 3:00, usiku kwa wasanii wa Bongo kufanya 'mavituzi' ya kutisha jukwaani ambapo Ben Pol, alianza kuimba 'laivu' na baadaye Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’.

Kwa ujumla Jay Dee, aliwakuna vilivyo P Square, akimba nyimbo zake zote kali na baadaye kumalizia na Joto Hasira huku ghafla Profesa Jay, akivamia jukwaa na kuungana naye katika kibao hicho kilichowafanya mashabiki kulipuka kwa shangwe kubwa zisizo kifani.

Mashabiki wa Bongo Fleva, walituliza 'mtima' wao usiku huo wakifurahia ladha tamu za 'laivu' pasipo chenga.

Joh Makini ndiye aliyefungua pazia kwa wasanii wa Bongo Flava.

Baada ya ladha hizo za Kibongo, ilifika zamu ya P Square kufanya kile kilichowafanya Watanzania kuhudhuria kwa wingi Leaders Club kwa kulitanguliza Kundi la wapiga vyombo wakiwamo Papii Jay (Drums), Mike (gitaa la solo), Mackay (mpiga kinanda) na Doyuu (mpiga gitaa la besi), waliopanda kuweka mambo sawa.

Majira ya saa 7:32, P Square walipanda jukwaani na kupiga vyombo wenyewe wakisindikizwa na mdundo wa wimbo wa Do Me, kisha wakaanza na ule wa Temptation na kisha kuendelea kukamua vilivyo.

Wakali hao hawakuonyesha kuchoka kwani waliendelea kukamua vibao vyao mbalimbali vikiwamo Roll It, Forever, kabla ya kuwashika vilivyo mashabiki kwa kuimba wimbo wa kiswahili wa wasanii wa Uganda, Radio & Weasel unaokwenda kwa jina la Nakudata.

Wasanii hao walizikdi kuwashika vilivyo Wabongo baada ya kuanza kutunishiana mizuli kwa kuonyesha mbavu, ambapo Paul alifanya kituko cha aina yake baada ya Peter kumuonyesha unene wa mbavu zake, yeye aliamua kushusha suruali yake yenye rangi nyekundu kidogo na kuwaonyesha mashabiki wake...!

"Hakika hele yetu imekwenda kihalali, hata kama ingekuwa laki moja ni sawa kabisa. Ilitakiwa mashabiki wa mikoani nao wapate burudani hii wajionee wenyewe badala ya kusimulia," alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Pinto.