come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ISHARA YA KIDOLE YAMFIKISHA MAHAKAMANI WILSHELE

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere ameshtakiwa kwa kutoa ishara za kuudhi akitumia mkono wake baada ya mechi ambayo viongozi hao wa Ligi ya Premia walilimwa 6-3 wakiwa Manchester City Jumamosi, FA ilisema.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anadaiwa kutoa ishara hiyo ya kuudhi akiielekeza kwa mashabiki wa City katika uwanja wa Etihad.

Kisa hicho hakikigunduliwa na marefa lakini kilinaswa kwenye video na Wilshere amefunguliwa mashtaka na FA chini ya mpango mpya unaofanyiwa majaribio wa kuchukua hatua kutokana na ‘visa visivyoonekana’ kwenye mechi za Ligi Kuu ya Uingereza.

“Chini ya mpango huo mpya, ikiwa tukio halikuonekana na marefa wanaosimamia mechi, basi jopo la watu watatu litaomba na FA kuchunguza tukio hilo na kupendekeza hatua ambayo wanadhani refa alifaa kuchukua kama angeshuhudia tukio hilo wakati huo,” FA ilisema kupitia taarifa Jumanne.


"Ili mchezaji afunguliwe shtaka na FA, wanachama wote watatu wa jopo hilo lazima waafikiane kwamba ni kosa ambalo linaweza kufanya mchezaji atimuliwe. Kuhusu kisa hiki, jopo lilikubaliana kwa kauli moja.