HATIMAYE mwanadada anayetamba kwenye kiwanda cha muziki wa kizazi kipya bongo Jdith Wambura maarufu Lady Jaydee ametambulisha sehemu aliyozaliwa kupitia ukurasa wake wa facebook mapema hivi karibuni.
Katika utambulisho huo, Jaydee ameweka wazi kuwa yeye alizaliwa Shinyanga katika mzingira ya umasikini tofauti na sasa ambapo ameibuka kuwa mmoja kati ya wasanii wenye fedha chafu, itazame kwa makini nyumba aliyozaliwa staa huyo.