come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

AZAM FC YAITAMANI SIMBA.

Na Fikiri Salum, Zanzibar

KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog ambacho tayari kimepata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup huko Zanzibar kimeonyesha dhamila yake ya kutaka kukutana na Wekundu wa Msimbazi kwenye hatua yoyote.

Wachezaji wa timu hiyo wakijiamini kabisa wametamba kuwa wanaitamani sana Simba ili waionyeshe jeuri ya soka kwani wao ndio kiboko ya Simba, wachezaji hao pasipo kutaja majina yao wamedai kuwa Simba si lolote na ni nguvu ya soda tu ila wao watabeba ndoo kwa mara ya tatu mfululizo.


Naye msemaji wa timu hiyo Jaffar Maganga amesema kuwa Azam ni timu bora kabisa katika michuano hiyo  na ni lazima wachukue tena ubingwa, kuhusu Simba amedai yeye si msemaji wa Simba ila hawaiogopi na wako tayari kukutana nayo muda wowote wakipangwa nayo.