Shughuli ya kutafuta ndege ya abiria ya Malaysia
imeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya suitofahamu na
wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za watu waliopotea wakiwa katika ndege
hiyo.
Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za baharini kunakosemekana ndege ilipotelea mpaka maili 100.
Ndege iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege