Polisi Moro inayonolewa na kocha Richard Adolph ilikuwa ikihitaji ushindi wa namna yoyote katika mechi hiyo, ambapo dakika ya sita nahodha wake Nahoda Bakari alimimina krosi iliyomkutana na Mfuko Abdallah ambaye aliukwamisha mpira nyavuni.
Bao hilo liliwachanganya Majimaji na kusababisha mambo yawaendee kombo kwani dakika ya 26 waliruhusu kufungwa bao la pili na, James Mganda anayechezea timu ya taifa ya vijana (Serengeti Boys U17).
Mganda alifunga bao hilo baada ya kutumia vema pasi nzuri ya Nicolaus Kabipe.
Kipindi cha pili Majimaji inayonolewa na kocha Hassan Banyai ilikianza kwa nguvu, ambapo ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 79 lililofungwa na Anthony Mwingira.