|
|
Matokeo hayo katika musururu wa mechi la ligi ya Premier ya Uingereza yaliwezesha Spurs kudhibiti nafasi ya tano ingawa wana mwanya wa alama nne na Manchester City wanaorodheshwa nne ingawa wamecheza mechi mbili zaidi.
Masikitiko ya Cardiff yalizidi kuongezeka kwani kuchakazwa ugenini kwa mara saba mfururizo kunamaanisha wanabaki alama tatu nyuma ya timu inayomiliki nafasi ya mwisho ya kuhakikisha hadhi ya Premier.
Majonzi yao yalisababishwa na Soldado amabaye amepata shinikizo kali kwa kulegea katika harakati za kupata mabao huku taarifa zikidokeza atatemwa baada ya musimu mmoja pekee.
Straika huyo wa Uhispania alilipa imani kuu ya mwalimu wake Tim Sherwood pale alipofunga bao la ustadi katika kipindi cha kwanza lililotosha kunyakua ushindi baada ya pilka pilka za mechi hiyo.
Kiungo wa pembe, Andros Townsend alianzisha mchezo uliozaa bao alipookota mpira wa juu juu kutoka kipa wake, Hugo Lloris kabla ya kumpata mshambuliaji wa Togo, Emmanuel Adebayor kushoto mwa uwanja.
Adebayor alidhibiti mpira hadi Soldado alipoingia kwenye eneo la hatari na kasha kumuunganishia straika mwenzake fursa ya kufunga ambayo aliitumia kwa ustadi mkuu kwa kuwalemea walinda ngome watatu wa Cardiff na kumfunika kipa wao David Marshall kwa kombora safi.
Kwingineko, straika matata wa Ubelgiji, Christian Benteke, alipata magoli mawili kuinua timu yake Aston Villa kukamilisha ushindi wa 4-1 ambao walijipata taabani pale wageni wao Norwich City walipofungua ukurasa wa mabao.
Mambo yalionekana kuendea wenyeji kombo pale Wes Hoolahan alipofungia Norwich dakika tatu pekee baada ya kipenga cha mwanzo kabla ya Benteke kujibu kupitia kombora mzito dakika ya 25 kabla ya kupata lake la pili kwa kichwa kabla ya wapinzani wao hawajapumua.
Leandro Bacuna na bao la kujifunga wenyewe kutoka Sebastian Bassong walikamilisha ufungaji.
Crystal Palace walilazimisha sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji Swansea kukamilisha orodha ya Jumapil