come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAN CITY, LIVERPOOL WAANZA KWA KISHINDO PREMIA

Daniel Sturridge

Manchester City na Liverpool, waliomaliza nambari mbili za kwanza Ligi ya Premia msimu uliopita, walitolewa jasho na wapinzani wao kabla ya kuanza kampeni zao kwa ushindi Jumapili.

David Silva na Sergio Aguero walifungia City na kuwapa ushindi wa 2-0 wakiwa Newcastle United, Daniel Sturridge akiwa awali amefunga dakika za mwisho na kuwapa Liverpool ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Southampton.

Meneja wa City Manuel Pellegrini alimtunuku kiungo wa kati Mbrazil Fernando mechi yake ya kwanza na akashuhudia timu yake ikienda kifua mbele dakika ya 38 uwanjani St James' Park.

Yaya Toure alimpata Edin Dzeko kwa pasi ya juu na madifenda wa kati wa Newcastle walipokuwa wakikimbia, Mbosnia huyo akaunganishia mpira Silva kwa kisigino na Mhispania huyo akambwaga Tim Krul kwa urahisi.


Nguvu mpya wa Newcastle Ayoze Perez kisha alishuhudia kombora lake la kujipinda likipinduliwa na Fernando na kutolewa nje, kabla ya Aguero kuchomoka na kumbwaga Krul jaribio lake la pili dakika za mwisho na kuua mechi hiyo.

Awali, Sturridge alifungia Liverpool bao la ushindi dakika ya 79 dhidi ya Southampton katika uwanja wa Anfield uliokuwa umelowa maji.

Raheem Sterling aliweka Liverpool kifua mbele katikati ya kipindi cha kwanza, lakini Clyne akakomboa muda mfupi baada ya saa ya mchezo baada ya kubadilisha pasi safi na mgeni Dusan Tadic.
Vijana hao wa Brendan Rodgers walionekana kuelekea kupoteza alama mechi yao ya kwanza ya ushindani tangu wamuuze Luis Suarez kwa Barcelona, lakini kukiwa na dakika 11 zilizosalia za kucheza, Sterling alionana vyema na Sturridge aliyefunga bao la ushindi.