Breaking News....Simba, Yanga hatihati kushiriki Kagame Darfur
MABINGWA
watetezi wa kombe la Kagame Yanga na mpinzani wake wa jadi Simba
wakashindwa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati
maarufu kama kombe la Kagame ambayo itafanyika nchini Sudan, Kwa mujibu
wa msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga, Amesema kuwa hali ya Sudan
kwa sasa si shwari hivyo serikali imetilia shaka ushiriki wa vilabu
hivyo.
Akiwa
ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook, Kamwaga amesema kuwa Huenda
michuano hiyo isiwe na timu za Tanzania kufuatia serikali kushutushwa na
usalama uliopo, 'Sudan hakuna usalama kwani ili uweze kuishi huko kwa
siku hizo chache lazima ujikinge na mavazi ya kuzuia silaha', alisema
Kamwaga.
'Serikali imesema haioni busara ya Kagame Cup kupigwa
Darfur Hakuna hoteli ya maana na watu wanashauriwa kutembea na
fulana zinazozuia risasi kupenya ilisema taharifa hiyo