Mshambuliaji mpya wa Simba, Amissi Tambwe (Pichani) , jana
usiku alitarajiwa kurejea kwao Burundi kwa ajili ya kuitumikia timu yake
ya taifa katika mechi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za
Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Sudan
itakayofanyika keshokutwa Jumatano mjini Bujumbura.
Tayari mfungaji bora huyo wa zamani wa mabingwa wapya wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Vital'O ameshasaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba.
Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema kuwa mshambuliaji huyo atarejea nchini Alhamisi kwa ajili ya kuanza mazoezi na wachezaji wenzake wanaotarajiwa kuitumikia klabu hiyo katika msimu huo wa mwaka 2013/ 2014.
"Tulimalizana naye na sasa tumeshafikisha wachezaji wanne wa kigeni," alisema Mtawala.
Aliwataja wachezaji wengine wa kigeni ambao tayari wameshasajiliwa kwa ajili ya msimu ujao kuwa ni pamoja na Waganda watatu, kipa Abel Dhaira, beki wa kati Samuel Ssenkoomi na kiungo Mussa Mudde.
Aliongeza kuwa wanaamini wachezaji hao wakigeni ambao wana uzoefu na mechi za kimataifa watakisaidia kikosi hicho kwa ushirikiano na wachezaji wao chipukizi waliowapandisha kutoka Simba B.
Mchezaji mwingine wa kigeni ambaye huenda akakamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni ni Mganda Moses Oloya, ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Vietnam na mkataba wake umebakiza miezi mitatu ili umalizike.
Oloya anatarajiwa kusajiliwa na Simba katika kipindi cha dirisha dogo hapo Novemba mwaka huu.
Timu zote 14 zinazotarajiwa kushiriki Ligi Kuu ya Bara msimu ujao ambayo itafanyika kuanzia Agostu 24 mwaka huu ziko katika pilika za usajili kwa ajili ya msimu mpya.
Yanga ndiyo mabingwa wa msimu uliopita wakati Azam ilimaliza ikiwa ya pili na Simba ilishika nafasi ya tatu.