come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

CHEKA APANIA KUMDUNDA MMAREKANI

BONDIA mahiri nchini, Francis Cheka ‘SMG’, amesema atahakikisha anamsambaratisha raundi za mwanzo bondia Mmarekani Derrick Siembley katika pambano lao la kuwania ubingwa wa dunia lililopangwa kufanyika Agosti 30, mwaka huu.


Pambano hilo la raundi 12 uzani wa kati ‘Supper Middle’ linatarajiwa kufanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu akiwa mkoani Morogoro, Cheka alisema licha ya kutojua historia ya bondia huyo, atahakikisha anapigana kufa na kupona hadi kunyakua mkanda huo.

“Bondia huyo simfahamu na wala sijawahi kuisikia historia yake, mimi ni bondia ninayejiamini katika pambano lolote, naendelea na mazoezi ya kawaida tu, bado sijaanza mazoezi kwa ajili ya pambano hilo,” alisema Cheka.

Bondia huyo ambaye hana historia ya kupigwa katika mapambano yake mengi, amewataka Watanzania kumwagika kwa wingi siku hiyo ili kumpa hamasa zaidi ya kumpiga Mmarekani huyo.