KLABU ya Atletico Madrid imeanza mkakati wa kumsajili kwa Pauni Milioni 17.5, nyota wa Arsenal, Santi Cazorla.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Miguel Angel Gil Marin alikuwaa London
jana usiku kujaribu kukutana na Arsenal kwa ajili ya kiungo huyo mwenye
umri wa miaka 28.
Atletico
ina fedha za kutosha baada ya kumuuza Radamel Falcao klabu ya Monaco
Pauni Milioni 51 na wanafikiri Pauni Milioni 17.5 zitamfanya Arsene
Wenger awape Cazorla.
Wakati
Wenger na karibu kikosi chake chote kipo ziarani Vietnam, Cazorla
hayupo, baada ya kupewa muda zaidi wa kupumzika kufuatia kuwa na timu
yake ya taifa kwenye Kombe la Mabara.
Marin
alitarajia kuzungumza Dick Law, Ofisa wa Arsenal anayeshughulika na
uhamisho wa wachezaji na ambaye pia hajaenda ziara ya Mashariki ya mbali
na timu.
Atletico
ilitaka kumsaini Cazorla msimu uliopita kutoka Malaga, lakini haikufika
dau la Pauni Milioni 16.5 ambalo Arsenal walitoa.

Super Star: Cazorla alifanya vizuri Arsenal katika msimu wake wa kwanza, akifunga mabao 12 na kutoa pasi 16 za mabao
Lakini
baada ya kumnasa rafiki mzuri wa Cazorla, David Villa kutoka Barcelona,
klabu hiyo ya Hispania inataka kujiimarisha zaidi.
Hakuna
hakika kama Arsenal itakubali kumuuza mmoja katika ya wachezaji bora
kwa sasa- Cazorla aliyefunga mabao 12 na kutoa pasi 16 za mabao msimu
uliopita.
Wenyewe
wanataka kuimarisha kikosi chao kwa kuwasajili Luis Suarez au Gonzalo
Higuain, na si kupoteza nyota wake kama miaka iliyopita, lakini Atletico
wana matumaini fedha itazungumza.

Anatakiwa: Luis Suarez anatakiwa na Arsenal, ingawa dau la Pauni Milioni 40 linaweza kuwarudisha nyuma
Wakala
wa Suarez amesema dau la kuuzwa mchezaji huyo ni kuanzia Pauni Milioni
40 ambaye inafahamika hafurahii maisha Liverpool na Arsenal ilikuwa
tayari kutoa Pauni Milioni 35.
The
Gunners pia inaweza kujaribu bahati yake kwa Wayne Rooney ambaye
inaonekana ana shaka ya kuwasilisha barua ya maombi ya kuondoka
Manchester United, ingawa anatakiwa pia na Chelsea iliyoonyesha nia ya
dhati ya kumng'oa Old Trafford.
Arsenal inajiandaa kucheza mechi nyingine katika ziara yake Vietnam leo.

Uwekezajaji kwa Mspanyola Villa: David Villa (wa pili kulia) akifanya mazoezi wenzake katika timu mpya, Atletico Madrid
