come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NYOTA TISA STARS WAMTIA HOFU MICHO

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’, Sredejovich Milutin ‘Micho’, amesema anatarajia mechi ya kesho dhidi ya Taifa Stars itakuwa ya ushindani hasa ikizingatiwa Tanzania ina nyota walioonesha soka safi katika mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwakani, dhidi ya Ivory Coast hivi karibuni.


Akizungumza mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, Micho alisema Stars ina nyota tisa walioonesha uwezo kwenye mechi hiyo, hivyo anategemea mechi ya ushindani.

Micho alisema, ana imani mchezo utakuwa mzuri na wa kuvutia huku akisisitiza kuwa timu ambayo itacheza vizuri ndiyo itakayoshinda.

Aliongeza kuwa hata yeye amekuja kwa ajili ya kushinda ila lolote linaweza kutokea, kwani nao wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mchezo huo wa mchujo kusaka tiketi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN).

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Stars, Marsh Sylvester, alisema kutokuwapo kwa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ambao wanacheza soka ya kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Afrika Kusini ni pengo, lakini watawatumia washambuliaji Mrisho Ngasa na John Boko, ambao ana imani hawatawaangusha Watanzania.

“Tumejipanga vya kutosha, ila ‘gape’ la Samatta na Ulimwengu linaonekana, lakini hakuna jinsi, si wachezaji wa ligi yetu na katika safu ya ulinzi tuko vizuri, bali ushambuliaji ndio tunazidi kuimarisha,” alisema.

Wakati Stars haikuwa na programu ya mazoezi jana, wapinzani wao walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, wakati leo saa 9:00 watakuwa Uwanja wa Taifa, kabla ya kuipisha Stars itakayoanza mazoezi saa 10:00 jioni.

Wachezaji wanaounda The Cranes ni makipa; Ismail Watenga, Kimera Ali na Muwonge Hamza; mabeki ni Guma Dennis, Kasaaga Richard, Kawooya Fahad, Kisalita Ayub, Magombe Hakim, Malinga Richard, Mukisa Yusuf, Savio Kabugo na Wadada Nicholas.

Viungo ni Ali Feni, Birungi Michael, Frank Kalanda, Hassan Wasswa, Kyeyune Said, Majwega Brian, Mpande Joseph, Muganga Ronald, Ntege Ivan na Owen Kasule, wakati washambuliaji ni Edema Patrick, Herman Wasswa na Tonny Odur.

Stars wapo Juma Kaseja, Aishi Manula, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Amri Kiemba, Athuman Idd ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Juma Liuzio, Mwinyi Kazimoto, Mudathiri Yahya, Salum Abubakar, Simon Msuva, David Luhende na Vincent Barnabas, Khamis Mcha, Agrey Moris, Erasto Nyoni, Kelvine Yondan, Nadr Haroub ‘Canavaro’, Shomari Kapombe, Mrisho Ngasa na John Boko.

Katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa, Uganda iko nafasi ya 80 huku Tanzania ikiwa ya 121