come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

RWANDA WENYEJI KAGAME, CHALENJI 2014

Mashindano yajayo Kombe la Kagame na Chelenji, yanatarajiwa kufanyika nchini Rwanda, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaaji, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Mashindano ya mwaka huu Kombe la Kagame yaliyojaa uvutano wa kiusalama, yalifanyika nchini Sudan, ambapo timu ya Vital ‘O’ ya Burundi ilitwaa taji.
“Kagame na Chalenji yatafanyika Rwanda kwa ajili ya maandalizi ya CHAN),” alisema Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye.