Union iliyo kambini Raskazoni, inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga ikijiandaa na Ligi Kuu msimu ujao unayotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Morocco aliuambia mtandao huu jana kuwa, tangu aanze mazoezi vijana wake wameonyesha kujituma na kufanya mazoezi kwa bidii.
“Nashukuru mazoezi yanakwenda vizuri, mpaka sasa
wachezaji wote wameripoti kambini, ushindani umeongezeka kama mnavyojua
kutokana na kuwepo kwa wachezaji wenye uwezo,” alisema Morocco. Alisema
uwepo wa wachezaji wapya ndani ya kikosi chake kumeongeza ushindani
mkubwa miongoni mwa wachezaji. Baadhi ya wachezaji wapya na wenye uzoefu
ni Haruna Moshi Boban, Uhuru Seleman na Juma Nyosso waliojiunga kutoka
Simba na Azam FC.