MABINGWA wa soka Tanzania bara Yanga (Pichani), leo inaingia dimbani kukabiliana vikali na vibonde wake URA ya Uganda katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga timu hiyo ambayo jana iliizamisha Simba mabao 2-1 katika mchezo mwingine wa kirafiki, Mchezo wa leo utakuwa muhimu kwa Yanga ambao watajaribu kuutumia kwa lengo la kutambulisha kikosi chake kipya.
Yanga ambayo ilianza vibaya ziara yake ya mikoani ambapo ilikwenda jijini Mwanza Shinyanga na Tabora na kushindwa kupata ushindi hata mmoja hivyo itakuwa na kazi ya ziada katika mchezo huo, Naye kocha msaidizi wa Yanga Ferd Felix Minziro ameuambia mtandao huu kuwa Yanga ina kila sababu ya kuibuka mshindi katika mchezo huo
