
Fm Academia
Msemaji wa bendi hiyo Kelvin Mkinga aliwataja wanenguaji hao kuwa ni Mariam Ziadane na Halima Messi ambao kwa sasa wanaendelea na kazi baada ya kurejea.
"Mimi siku zote huwa ninasema kuwa mwanamuziki wa bendi ya FM Academia hawezi kuhamia kwingine...ukiona yuko kwingine, basi ujue kuwa amekwenda kutembea kwa muda na kisha atarudi nyumbani," alisema Mkinga.
Alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikitokea kila mara kama ilivyojirudia kwa wanenguaji hao ambao sasa wameamua kurejea wakati bendi ikijiandaa kuzindua albamu ya 'Chuki ya Nini'.
Baadhi ya nyimbo za albamu hiyo ni: 'Fataki', 'Otilia', 'Neema', 'Ndoa ya Kisasa' na nyingine ambazo huporomoshwa katika maonyesho ya kila mwisho wa wiki.
Aidha, Mkinga aliongeza kuwa wakati huu wa mfungo wa Ramadhani bendi inaendelea na maandalizi ya uzinduzi huo ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi makali huku pia ikitoa burudani kwa siku tatu za mwisho wa wiki.