KOCHA Manuel Pellegrini jana alikuwa mwenye furaha baada ya timu yake, Manchester City kuanza vyema Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya wenyeji Viktoria Plzen katika kundi lao D lenye timu za Bayern Munich na CSKA Moscow.
Dakika 10 zilitosha kwa City kutengeneza ushindi mnono na sasa wanaelekea kwenye mchezo na mahasimu, Man United Jumapili wakiwa wenye kujiamini.
Edin Dzeko alifunga la kwanza dakika ya 48, Yaya Toure akafunga la pili dakika ya 53 na Sergio 'Kun' Aguero akakamilisha kazi dakika ya 58 kwa bao la tatu.
kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Toure (Javi Garcia 80), Fernandinho, Jesus Navas/Milner dk67, Aguero, Nasri, Dzeko/Negredo dk83.
Plzen: Kozacik, Rajtoral, Hejda/Hubnik dk66, Prochazka, Limbersky, Horava, Horvath, Petrzela, Kolar/Duris dk61, Kovarik, Bakos/Tecl dk84.
Dream start: Manchester City players celebrate their away win at Viktoria Plzen.