come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MGAMBO YAAPA KUIVUTA SHARUBU SIMBA LEO

Licha ya timu yake kufungwa mechi mbili za Ligi Kuu ya Bara na kushinda mechi moja tu na kujikuta ikishika nafasi ya tisa ikiwa na pointi tatu tu, Kocha wa Mgambo, Mohamed Kampira amesema kamwe Simba isitarajie mteremko katika mchezo wa leo.


Kampira ameuambia mtandao huu kwamba, timu yake ipo jijini Dar es Salaam tangu wikiendi iliyopita na wameshafanya mazoezi ya kutosha kuweza kuibuka na ushindi.

“Sitishwi na matokeo yaliyotokea huko nyuma wala ukubwa wa timu ninayopambana nayo (Simba), mimi kazi yangu nimeshaifanya na wachezaji wangu sasa wapo tayari kwa mchezo ninachosubiri ni muda ufike ili tucheze na Simba,” alisema Kampira.

Kampira alisema kikosi chake hakina majeruhi wa kutisha kwani wachezaji wote wanaweza kupambana katika mechi ya kesho. “Sina majeruhi wa kutisha kwani wapo wachache wanaosumbuliwa na majeraha madogo madogo ambayo yanaweza kuwafanya wacheze,” alisema Kampira.