come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MESSI KAMA RONALDO, AFUNGA HAT TRICK BARCELONA IKIUA 4

Lionel Messi amejibu mapigo ya mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid baada ya kuifungia hat-trick Barcelona katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Nou Camp.


Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique.

Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson.

Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.

Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72.

Ajax: Vermeer, van Rhijn, Denswil, Moisander/van der Hoorn dk73, Blind/Schone dk78, Poulsen, de Jong/Serero dk59, Duarte, Bojan, Sigthorsson na Boilesen.