Raha ya mechi bao: Michu akienda kwa
Jonjo Shelvey (kulia) kushangilia naye baada bya kuifungia bao la pili
Swansea dakika ya 64 ikimenyana na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu
ya England jana. Timu hizo zilitoka 2-2 bao lingine la Swansea
likifungwa na Jonjo dakika ya pili tu, wakati mabao ya Liverpool
yalifungwa na Sturridge dakika ya nne na Moses dakika ya 36.
Kazi nzuri: Michu akishangilia baada ya kuifungia Swansea bao la pili
Shujaa: Jonjo Shelvey akishangilia baada ya kuifungia Swansea bao la kwanza
Kitu hicho: Shelvey akifumua shuti kufunga
Heshima: Steven Gerrard alivaa beji ya Unahodha Liverpool kwa mara ya 400
Babu kubwa: Shelvey akileta kizaazaa langoni mwa Liverpool
Mimi tena: Daniel Sturridge akiifungia bao la kusawazisha Liverpool, baada ya Shelvey kuifungia la kwanza Swansea
Anawarudisha kati: Wa mkopo kutoka Chelsea, Victor Moses amefunga katika mechi yake ya kwanza Liverpool
Jaribio zuri: Coutinho (kushoto) akibinuka tik tak mbele ya Wilfried Bony (kulia)
Kiulaini: Michu akifunga