come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

WAPINZANI WA YANGA KUWASILI


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDeBrQDoGrDLaNQLfC8I55CNoHJdOdwjKUO9RgOTxB_FL_a6gl4s0NZXi9qxHl_SmaVGmXMPXXEUrZtoCVpKANoKqUhOyPpKszU5qGUseeH46XemL6THBJCZxjbUR2xPOqes0gmnpMsb8/s1600/2.jpgWAPINZANI wa Yanga katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, timu ya Komorozine de Domoni kutoka Visiwa vya Comoro walitarajia kuwasili jana saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi yao ya kwanza itakayopigwa Uwanja wa Taifa Jumamosi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya Yanga mchana huu, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema wamepewa taarifa na Shirikisho la Soka (TFF) kuhusu ujio wa timu hiyo 'kibonde' na itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kesho.


Amesema kikosi cha Yanga chenye wachezaji 25 kimeweka kambi mjini Bagamoyo, Pwani kujiandaa na mchezo huo na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri wakiendelea na maandalizi ya mchezo huo wa Hatua ya Awali ya mshindano hayo makubwa kwa klabu barani Afrika.

Kizuguto amesema kocha wao Mholanzi Hans Van der Pluijm jana alikifanyisha kikosi chake mazoezi mara mbili asubuhi na jioni , huku leo wanaendelea na mazoezi jioni katika kujiweka sawa kwa ajii ya mehci hiyo ambayo kama wakifanikiwa kufuzu, watapambana na mabingwa wa Afrika, timu ya Al Ahly ya Misri.

Aidha, Kizuguto amesema kiingilio cha juu katika mchezo huo kitakuwa Sh. 30,000 kwa VIP A na Sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani na kwamba tayari uongozi wa timu hiyo ya Jangwani umeandaa tiketi 45,000 kwa ajili ya mchezo huo zitakazokuwa na vipande vitatu ili kudhibiti uchakachuaji.

"Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi (ijumaa), tumeamua kuandaa tiketi zenye vipande vitatu ili kuzuia uuzwaji wa tiketi feki, tunaomba mashabiki wanunue tiketi kwenye maeneo rasmi yaliyotengwa ikiwamo hapa makao makuu ya klabu," amesema Kizuguto.