MWANAMUZIKI aliyeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya Kill music Award 2014 Batarokota amedai video ya wimbo wake wa Kwejaga-nyangisha ndio ulioweza kumpaisha na kufikia hatua hiyo ambapo sasa atazidisha juhudi ili aweze kufahamika.
Batarokota amedai wimbo wake huo umebeba maudhui halisi ya utamaduni wa Kitanzania na ambao umechangia kumweka hapo halipo, Batarokota amesema kuwa mbali na kuanza muziki muda mrefu na kufanikiwa kuingiza nyimbo kwenye tuzo za kill kwa mara ya kwanza lakini ataendelea na mapambano.
Hata hivyo msanii huyo ameamua rasmi kuimba muziki wenye vionjo vya asili na kuachana na muziki wa kufokafoka ambao alikuwa akiufanya hapo kwanza, 'Hii ni nyimbo yangu ya kwanza ya kiasili ila nimeshawahi kutoa nyingi zenye mahadhi ya kizazi kipya', alisema na kuongeza.