come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DAVID MOYES AMUONYA MWAMUZI

KOCHA wa Manchester United, David Moyes amemuambia refa wa Hispania, Carlos Carballo kutoa maamuzi sahihi katika mchezo wao dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich kutokana na tabia ya wachezaji wa timu hiyo kujirusha kujiangusha.

United inatakutana na mabingwa wa Bundesliga leo Uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa kwanza wa kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bayern inapewa nafasi kubwa ya kushinda, lakini timu hiyo ya kocha Pep Guardiola ilishutumiwa baada ya kuitoa Arsenal katika raundi iliyopita, kwa Arsene Wenger kumlaumu Arjen Robben kuwa hodari wa kujirusha kujiangusha.


Moyes alisema: "Tunawaamini marefa watafanya uamuzi sahihi. Kujirusha ni moja ya vitu vibaya vya kufanyia kazi. Ningependa kutahadharisha juu ya hilo, lakini nisingependa kumlenga mchezaji binafsi,".

United imekuwa ikiumizwa na maamuzi ya marefa siku za karibuni katika michuano ya Ulaya, na winga Nani alitolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Real Madrid mwaka jana wakati beki Rafael alitolewa pia dhidi ya Bayern mwaka 2010.

Wajerumani hao tayari wamekwishatetea ubingwa wa Bundesliga na wameshinda mechi zao 27 kati ya 30 zilizopita kwenye mashindano yote. Lakini Ryan Giggs bado anaamini United inaweza kufika fainali.