Liverpool itaipiku Manchester City katika nafasi ya pili msimu huu.
Kocha Brendan Rodgers anasema iwapo kikosi chake kitaendelea na kasi walionayo kwa sasa Liverpool itamaliza katika nafasi ya pili.
Rodgers aliyasema hayo baada ya Liverpool kusajili ushindi wake wa tano mfululizo ilipoilaza Swansea 1-0 jumatatu usiku
Bao la pekee katika mechi hiyo ilipachikwa kimiani na Jordan Henderson .
Liverpool inashikilia nafasi ya 5 hivi sasa katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza wakiwa wamesalia na mechi 9 za kuchezwa msimu huu.
The Reds wamejizolea alama 54 alama nne tu nyuma ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Manchester City.
Vijana wa Mancini waliambulia kichapo cha bao moja kwa nunge mikononi mwa Burnley mwishoni mwa juma.
"Baada ya matokeo ya Manchester City dhidi ya Burnley ninahakika tuko katika nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi ya pili,"alisema Rodgers.
"Motisha wetu hivi sasa uko juu na hivyo itatusaidia kukabili mechi zetu zote zilizosalia."
Liverpool haijashindwa katika mechi 13 za ligi ya Premia
Iwapo Liverpool wanajiandaa kuchuana na Manchester United, jumapili ijayo huku wakitafuta ushindi iliwawapiku kutoka nafasi ya nne.
"tuko tayari'' alisema naibu nahodha wa the Reds Henderson.
"Najua kuwa itakuwa mechi ngumu lakini haidhuru Anfield ni kwetu tutajitahidi tuzoe alama zote"
Liverpool ilikuwa inashikilia nafasi ya 10 mwezi Desemba ilipoambulia kichapo cha 3-0 Old Trafford lakini tangia wakati huo timu hiyo imeshinda mechi 13 za ligi ya premia.
Ni timu ya Chelsea pekee ambayo imeweza kusajili msururu bora zaidi wa matokeo .
The Blues wameshinda mechi 14 bila kushindwa.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako