Mbrazil wa Yanga, Andrey Countinho ameanza mazoezi mepesi na timu yake katika kile kinachoonekana kuimarika kwa hali yake ya goti.
Countinho aliumia wiki kadhaa zilizopita na alishindwa kusafiri katika safari ya Yanga ya kuelekea Gaborone, Botswana wakati Yanga ilipokuwa inacheza mechi ya marudiano na BDF XI ya nchini humo.
Kufanya mazoezi kwa kiungo huyo kunaleta matumaini kwa Yanga kumtumia katika mechi zake za ligi kuu na zile za Kombe la Shirikisho barani Africa, kwa mujibu wa kocha msaidizi, Charles Boniface Mkwasa.
Countinho anasifika kwa uchezaji wake, hasa kwa upigani wa mipira ya adhabu.
Timu yake inakaribiwa na kibarua cha kuitoa Platinum FC ya Zimbabwe katika michuano hiyo ya Afrika ili icheze hatua inayofuata
Habari zinasema kuwa endapo Yanga itaitoa Platinum, yenye kibarua cha kushinda baada ya kufungwa 5-1 Dar es Salaam, itacheza na moja ya klabu kongwe na yenye uzoefu, Etoile du Sahel ya Tunisia au au S.L Benfica ya Angola katika hatua inayofuata